- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya wilaya ya Ngara hivi karibuni imekamilisha zoezi la kuwapiga chapa ya moto Ng’ombe lililolenga kuwatambua wafugaji, kudhibiti wizi, utoroshaji na uhamishaji horera wa mifugo kutoka eneo moja kwenda jingine.
Afisa Mifugo na Uvuvi wa wilaya ndugu Josephat Sangatati amesema kuwa zoezi hilo limekamilika na kuongeza kuwa kwa sasa kinachoendelea ni kupiga chapa wale ng’ombe ambao chapa za moto zimefutika au zimefifia.
“Tulisajili wafugaji 5,184 wenye ng’ombe 77,058, lakini waliopigwa chapa ya moto ni ng’ombe 67,713 kwa sababu kulikuwa na ndama wa umri chini ya miezi sita amabao kisheria hawaruhusiwi kupigwa chapa.” Alisema Ndugu Sangatiti.
Aidha, amewakumbusha wafugaji wote wilayayani humu kuzingatia sheria ya wanyama ya mwaka 2013 inayowataka kutowahamisha mifugo waliosajiliwa kutoka eneo moja kwenda jingine, huku akiwataka kuzingatia sheria ya maeneo ya malisho na rasilimali za vyakula vya mifugo namba 13 ya mwaka 2010 inayokataza kuingiza mifugo nchini kutoka nje ya nchi.
Hata hivyo amesema kuwa ng’ombe wa maziwa ambao wanasubiri utambuzi wa kutumia herein za masikio kumepunguza asilimia za malengo waliojiwekea.
Ameongeza kuwa zoezi hili halikukamilika kwa wakati kwa sababu ya mvua nyingi zilizokuwa zikinyesha na upungufu wa baadhi ya vitendea kazi kama vile vibanio katika maeneo kadhaa.
Zoezi la kupiga ng`ombe chapa ya moto katika Halmashauri ya wilaya ya Ngara lilizinduliwa rasmi na mkuu wa wilayaya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele Novemba 27. 2017 katika kijiji cha Kasulo kata ya Kasulo na kuhitimishwa Januari 25, 2018 katika kijiji cha Bukiriro.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa