- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe.Ndaisaba George Ruhoro amewataka Wananchi wote wenye namba za NIDA kuwa, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
imekamilisha na kufikisha Vitambulisho 35,000 vya Uraia kwa Wananchi wa Jimbo la Ngara ambao tayari wana namba za NIDA.
Vitambulisho vitapelekwa kwa Watendaji wa Kata na Vijiji ili iwe rahisi kwa Wananchi kuvipata vitambulisho hivyo. Aidha vitambulisho vitatakiwa kuchukuliwa na Wananchi ndani ya siku 14 tu na baada ya hapo vitambulisho vitarejeshwa makao Makuu ya NIDA Wilayani.
Mhe Ndaisaba anawaomba Wananchi wenye namba za NIDA kufika kwenye Kata zao ili kuona kama na wao ni miongoni mwa waliopata Vitambulisho hivyo kwa awamu hii ili kuchukua vitambulisho vyao.
Zoezi la ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa Wilaya ya Ngara linatarajiwa kuzinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe.Kanali Mathias Kahabi, Mnamo 1/11/2023 kwenye eneo la Nazareth, Kata ya Ngara Mjini.
Kufika kwa Vitambulisho hivyo ni utekelezaji wa ahadi ya Mhe. Ndaisaba George Ruhoro aliyoitoa nyakati tofauti tofauti Jimboni ambapo aliahidi kufuatilia na kuhakikisha angalau Serikali inatoa vitambulisho 45,000 kufika mwishoni mwa mwaka 2023.
Mhe Ndaisaba Ruhoro anawajulisha Wananchi wote kuwa ameendelea kuomba Fedha zitakazowezesha NIDA pamoja na UHAMIAJI kurudi kwenye kata, ili kuandikisha Wananchi wapya ambao walipitwa kwenye mazoezi yaliyopita ya uandikishaji ili kupata vitambulisho vya Taifa. Awamu nyingine ya kuandikisha Wananchi inatarajia kufanyika mapema 2024.
Mhe. Mbunge anawapongeza viongozi wote wa Serikali wakiwemo Madiwani, watendaji wa kata na vijiji kwa kazi nzuri wanayoifanya na kwa utayari wao wa kuhakikisha kila Mtanzania wa Ngara anapata kitambulisho cha Taifa.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa