- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo limefanyika zoezi la usafi Wilayani Ngara ,ambapo Kila kiongozi alipopangiwa alielekea kwenye eneo lake hapa Ngara Mjini na kwenye Kata zingine wasimamizi viongozi Ngazi za Kata.
Zoezi hilo ambalo hufanyika Kila Alhamis ya wiki Kwa kufanya usafi wa Mazingira Maeneo ya Makazi, kwenye Ofisi mbalimbali, Maeneo ya Biashara pamoja na Mitaa zikiwemo mifereji /Barabara.
Zoezi hili la usafi wa Mazingira lilianzishwa na kuzinduliwa na Mhe Col Mathias J. kahabi Mkuu wa wilaya ya Ngara Kwa kushirikiana na Ndg Solomon Kimilike Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Ngara.
Akiongea Mhe Col Kahabi Amesema zoezi hili ni endelevu Kila vijiji,Mitaa, Kata , Mamlaka za miji Midogo. viongozi waendelee kusimamia ambapo timu Maalum ya ukaguzi itakuwa ikipita kukagua usafi .
Aidha aliwapongeza wananchi viongozi mbalimbali Kwa kujitoa kuhakikisha Ngara inang'aa . Mhe Col Kahabi alimalizia Kwa kusema Ngara kuwa safi na kung'aa inawezekana.
Eneo la Ofisi baada ya zoezi la usafi siku ya Alhamis leo.
Barabara kuu Ikiwa safi baada ya zoezi la usafi.
Maeneo ya Ofisi.
Zoezi la usafi.
Zoezi la usafi wa Mazingira Wilayani Ngara.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa