- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Limefanyika zoezi la usafi wa Mazingira na upandaji wa miti katika Kata 22 zilizopo Wilayani Ngara.
Zoezi la usafi kabambe na upandaji wa miti limefanyika Mamlaka ya mji Mdogo Rulenge.Ambapo zoezi Hilo lililoongozwa na kaimu katibu Tawala Wilaya Ndg.Jawadu s.Yusuph aliyemwakilisha Mkuu wa wilaya ya Ngara Kanali Matias Julius Kahabi , Ndg.Said Salum aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji Wilaya, Meneja TFS Ndg. Mussa Mlonga, Afisa Maendeleo ya Jamii, Afisa Mazingira, Afisa vijana,Afisa utumishi,Afisa utamaduni na michezo, wanafunzi na wananchi.
Zoezi la upandaji miti limefanyika shule ya sekondari Mubusoro Rulenge, Ambapo miti 509 imepandwa na miti 6,491 imepandwa Kata 22 Wilayani Ngara Ikiwa ni wiki ya maadhisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara kufikia 7,000.
Baada ya shughuli ya upandaji miti limefanyika zoezi la usafi kabambe Mamlaka ya mji Mdogo wa Rulenge pia Kwa Kata zote 22.
Meneja wa TFS aliwataka kutunzwa Kwa miti hiyo iliyopanda Leo na kuahidi kufanya ufuatiliaji Kata Kwa Kata Ili kuona hali ya miti hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya alimshukuru Meneja wa TFS Kwa ushirikiano mkubwa anaoutoa katika Wilaya ,Kwa Kutoa miti kwa Kata na Taasisi pasipo malipo.
Nae Kaimu katibu Tawala Wilaya aliwashukuru TFS Kwa Kutoa miti 7,000 Aidha alizitaka Kata zote zilizopatiwa miti kuhakikisha inatunza vizuri na Kutoa taarifa ya hali ya miti inavyoendelea.
Zoezi la Upandaji Miti 500 limefanyika shule ya Sekondari Mubusoro Mamlaka ya Mji mdogo wa Rulenge.
Wanafunzi wakisikiliza maelekezo Toka Kwa Meneja TFS kabla ya kupanda miti.
Kaimu katibu Tawala Ndg Jawadu Yusuph akipanda Mti kumwakilisha Mhe Mkuu wa Wilaya Ngara.
Zoezi la Upandaji miti likiendelea shule ya Sekondari Mubusoro.
Wakielekea maeneo ya kupanda miti.
Zoezi la kufanya usafi Rulenge.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa