- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ngara
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Kanali Mathias Julius Kahabi ameendelea na ziara ya kutembelea kata Mbalimbali za wilaya ya Ngara , kwa lengo la kufanya mikutano ya hadhara kwa kusikiliza na kutatua kero Kwa wananchi.
Mhe Mkuu wa Wilaya katika ziara hiyo aliongozana na kamati ya Usalama Wilaya, kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Emmanuely Kulwa, Wakuu wa Idara na Vitengo , Wakuu wa Taasisi za Serikali. NIDA, RUWASA, TARURA, TRA, TANESCO, Pamoja na Mhe Diwani kata ya Muganza ,uongozi wa kata na kijiji .
Mhe Mkuu wa Wilaya na timu yake wamefanya ziara Katika vijiji vya Mukubu na Muganza kata ya Muganza Wilayani Ngara.
Katika Mikutano miwili aliyofanya Mhe Mkuu wa Wilaya akitoa nafasi Kwa Idara Mbalimbali kutoa Maelezo ya Idara / Taasisi .
Wananchi wa Vijiji hivyo waliuliza kero zao na kupatiwa ufumbuzi na wataalam Mbalimbali waliofuatana na Mhe Mkuu wa Wilaya.
Mhe Mkuu wa Wilaya akiongea na wananchi amesisitiza
1. Wananchi wasiogope kuwasiliana na kuwa karibu na Mkuu wa wilaya Kanali Kahabi Kwa yeye ndiye Mwakilishi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.
2. Suala la Elimu Wazazi wasiwakatishe watoto masomo kwani Elimu husaidia kujikomboa na unyonyaji wa aina tofauti tofauti. Pia wanafunzi wote walioandikishwa kuanza la Kwanza na walishinda darasa la Saba na kuchaguliwa kwenda kidato Cha kwanza Wazazi wahakikishe wanakwenda Shule bila kuwaficha majumbani.Elimu ni ufunguo wa maisha
3. Lazima watoto waendelee na Elimu aliyosajiliwa na kuepusha Mdondoko wa wanafunzi kuanzia Msingi Hadi sekondari
4. Suala la ulinzi na usalama ni Jukumu la Kila Mwananchi.
5. Wananchi waache kufuga wahamiaji Kutoka nchi Jirani ni vyema kutii Sheria bila shuruti na upo utaratibu nzuri wa vibali vya Serikali Kwa raia wa kigeni.
Pamoja na yote hayo Mhe Mkuu wa wilaya amewashukuru viongozi wote Kwa kuendelea kushirikiana na kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji Wilaya, Kwa kuzidi kushirikiana pia Mhe Mbunge wa Jimbo la Ngara.
Mwisho ameomba wananchi kuendelea kuwa na Imani Kwa serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mama shupavu kabisa Rais na Amiri Jeshi mkuu Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.
Nae Mhe Diwani kata ya Muganza alimshukuru Mhe Mkuu wa Wilaya Kwa kufika kata ya Muganza kusikiliza na kutatua kero, Amempogeza Kwa utaratibu wa kufanya mikutano na kuongea na Wananchi.
Baadhi ya wataalam wa Halmashauri katika Mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero.
Wananchi wa kijiji cha Mukubu Kata ya muganza wakiwa kwenye Mkutano wa Hadhara wa kusikiliza na kutatua kero.
Wananchi wa Kijiji Cha Mukubu.
Kaimu katibu Tawala Ndg Jawadu Yusuph, Mwanasheria wa Halmashauri, na kaimu Afisa Elimu sekondari Bi Elina Yoweli katika mkutano wa hadhara kijiji cha Muganza.
Mkuu wa wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathias J.Kahabi aliyesimama akiongea na wananchi wa Kijiji Cha Muganza, ambapo wa kwanza kushoto ni Mhe Diwani Kata ya Muganza,wa pili kushoto ni kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg Emmanuely Kulwa pamoja na wataalam aliambatana nao.
Wananchi wa Kijiji Cha Muganza walivyojitokeza katika mkutano wa Hadhara kusikiliza na kutatua kero.
Wataalam Kutoka Halmashauri wakiwa kwenye Kikao hicho Kijiji Cha Muganza Kata ya Muganza Wilayani Ngara.
Wananchi.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa