- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wiki ya uwekezaji Kagera imefunguliwa leo tarehe 12 Agosti 2019 katika Ukumbi wa ELCT ulioko Manispaa ya Bukoba . Mwenyekiti alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguta. Kongamano hili lilihudhuriwa pia na Mabalozi wa Tanzania katika nchi za Congo, Rwanda,Uganda,Burundi na Kenya. Wakuu wa Wilaya zote za Kagera,Makatibu Tawala ,Wakurugenzi, Wafanyabiashara na Wadau mbalimbali walihudhuria pia.
Mkuu wa Mkoa alisema,"Mkoa wa Kagera umebahatika kuwa na fursa nyingi za kiuchumi. Nchi ya Tanzania imepakana na nchi sita ambazo inaweza kufanya nazo biashara moja kwa moja ambapo Kagera peke yake inapakana na nchi nne yaani Congo, Rwanda, Burundi na Uganda. Hivyo Kagera inatakiwa kuwa jukwaa la kufungua milango ya kuelekea kufikia soko la ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania".
Baada ya kufungua kongamano hilo,Mkuu wa Mkoa alitoa rai kwa wafanyabiashara kuitumia vyema fursa ya kupakana na nchi hizo nne kukuza uchumi wa kagera na Taifa kwa ujumla.
Katika uwasilisho wa taarifa za fursa zinazopatikana nchini Burundi,Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dr. Edmund aliwataka wafanyabiashara kujenga,kudumisha na kutumia mahusiano vizuri na wafanyabiashara wa Burundi maana Burundi inategemea sana bidhaa kutoka Tanzania. Hivyo Burundi itakuwa soko la Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Congo Lt. Jen. (Mstaafu) Paul I. Mella wakati wa taarifa yake alieleza kuwa Tanzania tuna fursa kubwa ya soko la mazo na bidhaa nyingi za viwandani. Pia aliwatoa hofu wafanyabiashara juu ya hali ya usalama na amani nchini Congo na kudai kuwa hali ni shari na salama hivyo wafanyabiashara wasipate hofu.
Balozi wa Tazania nchini Uganda Mh, Dk. Aziz P. Mlima alizungumzia fursa ambazo tunaweza kuzitumia nchini humo ikiwemo zao la parachichi ambalo Kagera tuna ardhi nzuri ya kustawi zao hilo. Pia alialika wawekezaji kuja kuwekeza katika sekta ya utalii mkoani Kagera maana ina vivutio vya muhimu na vya kuvutia.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya aliwaomba vyama vya biashara ikiwemo TCCIA na taasisi zingine za kibiashara ziwe msaada mkubwa kwa kutoa elimu juu ya ufanyaji wa biashara za kimataifa ikiwemo kufuata taratibu za nchi hizo.Balozi huyo alisema,"Kabla ya kuchukua fursa nchi za jirani au za nje ,wafanyabiashara mfanye takwimu,utafiti na kufuata taratibu za kibiashara katika nchi hizo ili kukwepa usumbufu".
Balozi wa Tanzania nchini Rwanda naye aliomba kujengwa kwa masoko ya mpakani ili kurahisisha upatikanaji wa bidhaa za wenda nchi jirani kwa ukaribu.
Mwisho Mwenyekiti wakati akihitimisha,aliwashukuru Mabalozi kwa kuitikia mwaliko huo wa kuja kuelezea wafanyabiashara juu ya fursa zilizopo nchi hizo.Pia aliwaomba kuyafanyia kazi maneno yaliyoletwa na mabalozi pamoja na kujipanga kwa ajili ya kufanya ziara ya kwenda kutembelea nchi jirani kwa dhumuni la kujionea fursa hizo.Alimaliza kwa kusema,"Maneno pekee bila matendo hatuwezi kufika popote'.
KAGERA:Eneo La Kimkakati Kwa Uchumi Wetu Na Afrika Mashariki
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa