- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Mh. Wilbard J. Bambara akiongozana na Kamati ya Fedha,Utawala na Mipango wametembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika wilaya ya Ngara. Katika ziara hiyo kamati hiyo ilitembelea jumla ya miradi kumi na saba (17) inayotekelezwa katika kata saba (07) za Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Miradi hiyo iliyotembelewa ina jumla ya Tsh 7,675,260,694.69 na imefikia katika hatua mbalimbali za utekelezaji katika mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo tisa (09) imekamlika na mingine iko katika hatua za umaliziaji.
Kamati hiyo ilipongeza juhudi zinazofanyika katika usimamizi wa miradi iliyokamilika na kuelekeza wataalam waendelee kusimamia miradi ambayo haijakamilika kwa weredi ili wananchi waweze kuitumia miundombinu hiyo kama shule,zahanati na hospitali zinazojengwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti alielekeza pia miradi iendelee kutekelezwa kwa kuzingatia taratibu zote za serikali za uendeshaji wa miradi ili iweze kukamilika kikamilifu na pia taratibu za fedha ziendelee kuzingatiwa na malipo yafanyike kwa wakati ili isitokee miradi kukwama au kuchelewa kisa malipo. Mkurugenzi Mtendaji aliahidi kuendelea kuzingatia taratibu za utekelezaji wa miradi na kusema kuwa miradi ambayo haijakamilika itakamilika kwa wakati na usahihi.
Aidha katika majumuisho ya ziara hiyo Mheshimiwa Mwenyekiti alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Samia Suluhu kwa kuendelea kuleta fedha kwa ajili ya miradi ya Maendeleo inayojumuisha ujenzi wa shule, zahanati na hospital kwa ajili ya Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.Pia Mheshimiwa mwenyekiti alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndg. Solomoni Kimilike kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ambayo yanachangia katika ujenzi wa miradi ya maendeleo pia.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa