- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Tarehe 05/9/2023,
Kamishna wa Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya Tanzania Mr Areta Lyimo, katika Ziara yake amefuatana na Viongozi Waandamizi Ndg Florence Kalambi na Ndg Suzan Lyakundi na kupokelewa na Col. Mathias Kahabi Mkuu wa Wilaya ya Ngara, kwa lengo la kutembelea na kukagua udhibiti wa madawa ya kulevya katika mipaka ya Kabanga na Rusumo.
Ikiwa ni pamoja na kutoa Elimu kwa Kamati za Usalama zilizoko katika Mipaka hiyo ya namna ya Kupambana na kudhibiti dawa za kulevya na Madhara yake,
Sheria zilizopo kuhusu mapambano na udhibiti wa Dawa za kulevya na Ushirikishwaji wa Jamii katika mapambano hayo.
Akiwa Ofisini kwa DC Ngara Col Mathias Kahabi alifanya mazungumzo ambapo alitoa maelekezo na maagizo Mbalimbali,
Aidha, Kamishna Lyimo ameagiza Kamati ya Usalama Wilaya kuhakikisha wanasimamia na kudhibiti vijana kutojiingiza kwenye swala la matumizi haramu ya Dawa za kulevya ambapo vijana wengi ambao ni nguvu kazi ya Taifa wanajiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya na kuleta athari kubwa Kijamii, Kiuchumi na Kiutamaduni.
Pia. Kamishna Lyimo, amesisitiza wale wanaojihusisha na dawa za kulevya ikiwemo Bangi operesheni maalum ifanyike ili kuhakikisha watu hao wanapatikana na kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria.
Watu hao ni pamoja na wanaolima, kusafirisha, kuuza na watumiaji bangi mijini na vijijini.
Mkuu wa Wilaya Mhe . Col Mathias Kahabi amemuahidi Kamishna Areta Lyimo kusimamia na kutekeleza maagizo hayo mapema iwezekanavyo kwa kushirikiana na Kamati ya Usalama Wilaya, Viongozi wa Halmashauri, Viongozi wa Chama Tawala(CCM) Viongozi wa dini Wilayani, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Vijijini, Wenyeviti wa Vijijini na Vitongoji pamoja na Wananchi wote wilaya ya Ngara.
#kazii endelee
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa