- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wanafunzi wa darasa la saba wameungana na wanafunzi wengine wa darasa la saba nchi nzima kufannya mtihani wao wa mwisho wa Taifa wa kumaliza elimu ya msingi. Mtihani huo ambao ni wa siku mbili umeanza leo tarehe 6 Septemba kwa masomo ya English, Hisabati na Kiswahili na utamalizika kesho tarehe 7 Septemba kwa masomo ya Maarifa na Kiswahili.
Akiongelea jinsi zoezi la mtihani linavoendelea, Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya Ndg Aidan John Bahama amesema jumla ya wanafunzi 4826 ndio waliosajiriwa kufanya mtihani huo likiwa ni ongezeko la wanafunzi 1185 kwa mwaka jana pia amesema tathmini ya wanafunzi ambao hawatafanya mtihani itatolewa mwishoni mwa zoezi zima. Watahiniwa hawa wanasimamiwa na walimu 482 waliopewa dhamana ya kuhakikisha hakuna udanganyifu katika mtihani huo.
Akizungumzia maoteo, Mkurugenzi mtendaji amesema kuwa kulingana na jinsi walimu walivyowaandaa wanafunzi hawa, wilaya inategemea kufikia ufaulu wa 89%.
Kwa maoteo hayo Mkurugenzi anawataka wazazi kuwaandaa watoto wao kisaikolojia ili wasirubuniwe kuolewa au kupata mimba hasa kwa watoto wa kike, kutoroshwa kwenda kufanya kazi za vibarua ama za ndani na mwishowe kukosa fursa ya kuendelea na masomo ya sekondari na hapa amewakumbusha wazazi kuwa elimu ya sekondari za serikali ni bure, cha msingi wajiandae kwa ajili ya matumizi madogo madogo ya watoto wao.
Aidha Mkurugenzi amesisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wazazi ambao watoto wao watafaulu na wasipelekwe kujiunga na masomo ya sekondari.
Awali, Afisa Elimu Shule za msingi Ndg Gideon Mwesiga amewaasa wahitimu kuendelea kuwa watulivu huko waendako kama walivoonesha katika kipindi hiki cha mtihani wao wa mwisho.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa