- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Tulikadiria kununua tani 500 za kahawa aina ya Alabaika, lakini tumekwishanunua tani zaidi ya 900, huku wakulima bado wana kahawa nyingi majumbani, na tunatarajia kukusanya zaidi ya tani 1000 msimu wa 2017/2018.” Alisema Meneja wa Ngara Farmers Corporative Ndugu Amphrey Katakweba.
Ndugu Katakweba aliyasema hayo wakati akiwakirisha mada Septemba 07, 2018, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ngara, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri, kujadili utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho Januari - Juni 2018.
Amesema mwanzoni walifanya maksio ya chini, hivyo walipata fedha kidogo za kukusanyia kahawa hiyo, ikilinganishwa na hali halisi ya kahawa ya Alabika, waliyozalisha wakulima katika msimu wa huu.
Alisema chama hicho kimepokea shilingi milioni 600 kwa ajili ya kuendelea kukusanya kahawa; huku akisistiza kuwa uenda na hiyo fedha isitoshe kukusanya kahawa yote ya wakulima, kwani bado kahawa ni nyingi vituoni.
Amekiri kuwa kahawa ya mkoa wa Kagera hasa ile ya wilayani Ngara, ina ubora mzuri sana kwa kuwaaarika wajumbe wa kikao hicho kwenda gharani kujionea; huku akiwaomba kumsaidia kutatua changamoto ya upungufu wa maghara ya kutunzia kahawa inayokusanywa.
“Waheshimiwa wajumbe nina wasiwasi wa ghara la kutunzia kahawa tunayokusanya, kwani sehemu tunayotunzia kahawa yetu imejaa, na bado tunaendelea kukusanya nyingine; wakati huo huo, mvua zinaanza kunyesha.” Alisema Katakweba.
Aidha, amekiambia kikao hicho kwamba mfumo wa umeme ni mdogo ukilinganishwa na ukubwa au uwezo wa mashine za kukobolea kahawa, kwa hiyo, wanafanyakazi kidogo ikilinganishwa na mzigo wanaokusanya.
Amesema chama chake cha ushirika kimepoteza mapato, kwa kushindwa kukusanya kahawa katika kipindi cha miaka minane iliyopita, huku akiwataka wajumbe hao kukisaidia chama hicho, kutatua kero za wananchi, zilizomo katika uwezo wao.
Pamoja na maelezo hayo wajumbe walitaka kujua iwapo wakulima ambao hawakurejeshewa magunia yao baada ya kuuza kahawa; Meneja huyo aliwahakikishia wajumbe hao kuwa kwa sasa chama akina gunia, lakini zikifika watarejeshewa.
Amewataka wajumbe kumsaidia kuwaelimisha wakulima ambao si waaminifu, kwa madai kwamba baadhi ya wakulima wanaweka maparachichi, mawe na hata wengine wanaleta kahawa ambayo ni chafu sana.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa