- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ndugu Aidan John Bahama, amewapongeza watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), kwa kazi nzuri ya kuboresha maisha ya kaya masikini na kwa miradi ya maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji huyo Ndugu Bahama, ametoa pongezi hizo Mei 21, 2018, wakati wa semina ya wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, iliyoendeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III).
Amewataka wakuu hao wa idara kuwa wasikivu, watulivu na makini wakati wote wa semina hiyo, ili iwe ya manufaa kwao kama wataalamu, na kwa walengwa wanaotegemea msaaada wa kitaalamu.
Aidha, Afisa Ufuatiliaji-kukuza Uchumi wa Kaya Masikini wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) Ndugu Yohanes Nchimbi, amesema kwamba Mfuko wa Maendeleo ya Jamii unalenga kuongeza uwezo wa kuzalisha kipato cha kaya masikini.
“Tunapenda walengwa wetu waweze kujisimamia wenyewe kwa vipindi vya kati na muda mrefu, ili tuweze kuziba pengo lililopo kati ya walengwa wa mpango, na watoa huduma mbalimbali, zitakazowawezesha kuongeza uwezo wa uzalishaji hatu kwa hatua.” Alisema Ndugu Nchimbi.
Mfuko huo una mpango wa kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharimia mahitaji ya kaya za walengwa, kupitia utekelezaji wa uhawishaji fedha na ajira za muda, mpango wa kuweka akiba na kukuza uchumi, kuboresha miundombinu pamoja na kuwajengea uwezo.
Mafunzo hayo yatadumu kwa siku tano tangu Mei 21-25, 2018, na kuwashirikisha wakuu wa idara ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Waheshimiwa Madiwani, wagani pamoja na walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF III)
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa