- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 19/7/2024, Mhe Col Mathias Julius Kahabi Mkuu wa wilaya ya Ngara amefanya Kikao cha ndani na Viongozi wa Tembo Nickel kwa ajili ya kupata maendeleo ya mradi huo ambao uko hatua ya Ulipaji fidia kwa waguswa (PAPs).
Akitoa maelekezo ya kina ya maendeleo ya mradi wa Tembo Nickel, Afisa Mahusiano wa mradi huo Cde Moses Rusasa ametoa taarifa kwa Mhe DC Kahabi kama ifuatavyo;-
A.Jumla ya Waguswa wa Mradi ni 1339 katika Vijiji vitano.
B. Waguswa ambao tayari wameshalipwa ni 1262 sawa na asilimia 94 ya waguswa wote.
C. Waguswa ambao bado ni 77 tu sawa na asimilia 6 ya Waguswa wote.
D. Kiasi ambacho tayari kimeshalipwa ni Shs bilioni 26.6
E. Data hizi zimechukuliwa hadi tarehe 30/6/2024 na kazi nzuri inaendelea kwenye eneo la Mradi.
Mhe DC Kahabi amewapongeza Viongozi wa Tembo Nickel *Cde Moses Rusasa na Ndg Beata Kisaka* kwa taarifa za mara kwa mara kuhusu maendeleo ya mradi ambao hadi sasa unaendelea vizuri na changamoto nyingi zimeendelea kutatuliwa kwa Ushirikiano mkubwa wa Tembo Nickel, DED Ngara Ndg Solomon Kimilike, Ki Wilaya, Viongozi wa Tarafa, Kata na Vijiji vinavyoguswa kwenye mradi huu.
Ngara Kazi inaendelea.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa