- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Miradi tisa (9) yenye thamani ya zaidi ya shillingi bilioni mbili inatarajiwa kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi wakati wa mbio za mwenge wa uhuru tarehe 14 Aprili mwaka huu wilayani Ngara.
Hayo ni kwa mujibu wa Mratibu wa mbio za Mwenge wilaya Ndugu Said Salum wakati akiwaeleza Mwenyekitii wa Kikao cha maadalizi ya mwenge Lt. Col. Michael M. Mtenjele na wajumbe kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya.
Ameitaja miradi hiyo kuwa ni vyumba vinne (4) vya madarasa shule ya msingi Njiapanda – Kasulo, shamba bora la migomba (FIA) la Magereza Rusumo, Kikundi cha Ushonaji cha akina mama Rusumo Boarder, kikundi cha kusaidiana cha Vijana Tuinuane Bodaboda kilichoko Rusumo boarder na Barabara ya lami Ngara mjini.
Miradi mingine ni klabu ya kupinga, kupambana na Rushwa/ mimba uttotoni, UKIMWI iliyoko shule ya sekondari Shunga, pump mpya ya kusukuma maji iliyoko Ngara mjini, jengo la upasuaji, wodi ya wazazi, nyumba ya mganga na ugawaji vyandarua kwa wazee katani Mabawe pamoja na Kituo cha mafuta kilichoko Nakatunga.
Ndugu salum amewataja wafadhili wa miradi hiyo kuwa ni Serikali kuu iliyotaoa zaidi ya shilingi 1,021,216,000/=, Halmashauri ya wilaya shilingi 36,912,180/=, wahisani mbalimbali shilingi 17,800,000/= na wananchi shilingi 1,296,150,000/=.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa