- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa Kagera Hajat Fatma Mwassa amekabidhi Msaada wa Kibinadamu wa Chakula na Mahitaji kwa Wananchi wa Wilaya ya Muleba na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Omumwani iliyopo Manispaa ya Bukoba, kufuatia Majanga yaliyowasibu hivi Karibuni.
Msaada huo Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Kitengo kinachoshughulikia Maafa. Wahanga Wamekabidhiwa Mnamo Tarehe 12 Novemba 2023 na Mhe Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Wamekabidhiwa vifaa pamoja na chakula kwa Wahanga wa Mvua na Upepo iliyonyesha Siku chache zilizopita Mkoa wa kagera Wilaya ya Muleba, na kusababisha maafa pia Shule ya Wasichana ya Omumwani ikipatwa na Janga la Moto ulioteketeza Sehemu ya Bweni na Mali za Wanafunzi.
"Kipekee Tunashukuru Mama yetu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa msaada huu, na Vifaa vilivyotolewa, Wahusika watavigawa kwa hekima na Busara kulingana na Hali ya Wahitaji, Kipaumbele kiwe kwa wale Wenye Hali Duni zaidi na Wahitaji zaidi, lakini pia Kwa upande wa Shule ya Sekondari ya Omumwani nimeelekeza Mhandisi kuanza mara Moja Kazi ya Kusanifu na kuona namna ya kurejesha Hali kwa kuanza na Ukarabati wa Mabweni Mawili yaliyopata madhara, wakati tukijipanga Kujenga Mengine mapya Matatu". Amesema Mkuu wa Mkoa Mhe. Fatma Mwassa
Msaada uliokabidhiwa kwa Wananchi wa Muleba ni pamoja na Magodoro 150, Blanketi 150, Mikeka 150, Vyandarua 150, Sahani s so150, Madumu ya Maji (Lita 10) 150, Sabuni Boksi 17, Ndoo (Lita 10) 150, Chakula Tani 23.16
Kwa upande wa Shule ya Omumwani Sekondari, wao wamekabidhiwa Magodoro 60, Blanketi 60, Ndoo (Lita 10) 120, Vyandarua 60, Sahani 60, Vikombe 60, Sabuni Vipande 556.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa