- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo Tarehe 14/12/2023 Mhe Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathias J.kahabi ameendelea na ziara ya Oparesheni Sikiliza na kutatua Kero Kwa Wananchi.
Mkuu wa Wilaya alifuatana na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg. Solomon Kimilike, kamati ya Usalama Wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri,Wakuu wa NIDA,TARURA,RUWASA, TANESCO pia Uongozi wa kata ,Mtendaji kata, Afisa tarafa na Diwani Mhe. Niyonzoma Fabian.
Mkurugenzi Mtendaji aliwakaribisha Idara Mbalimbali kutoa Maelezo na iwapo Kuna kero iulizwe na kujibiwa akianza na Maji (RUWASA), Barabara TARURA, TASAF, AFYA, ELIMU, (BIASHARA,VIWANDA Na UWEKEZAJI), M/JAMII
Wananchi Waliuliza kero zao Mbalimbali hasa Kwa NIDA,Maji,Barabara, TASAF, Afya,Biashara,uwekezaji, Elimu Msingi na Sekondari.
Mhe Mkuu wa Wilaya alisisitiza Kwa wananchi wahakikishe wanawapeleka watoto shule Kwa Darasa la 1 na wanakwenda kuanza kidato Cha 1 .kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuwarahisishia wananchi Eliimu bule bila malipo pia Ujenzi wa vyumba vizuri vya madarasa.
Mhe Mkuu wa Wilaya alisisitiza suala la ulinzi na Usalama Rulenge ni Jukumu letu Sisi wote wananchi mmoja mmoja Kwa kushirikiana na Jeshi la polisi . Pia alikemea suala la wananchi kuwaleta wahamiaji Haramu bila kufuata sheria ni kosa, aliendelea Kwa kusema suala la uharifu kuwa polisi wapo ila uwepo ushirikiano mkubwa wa wananchi na Jeshi la polisi. Ambapo ocs Rulenge alisema mbele ya Mkuu wa Wilaya kuwa Sasa miaka 4 suala la uharifu limedhibitiwa Kwa raia na Mali zao Kwa Rulenge.
Mhe Mkuu wa Wilaya aliwataka wananchi Kwa kuwa ni Kipindi Cha mvua kunyesha kwenda kufanya kazi ya Kilimo ili kujipatia kipato Cha mmoja mmoja aidha aliwaonya wananchi wanaofanya Biashara ya Magendo waiache Biashara hiyo.
Wananchi wa Rulenge walimshukuru Mkuu wa Wilaya Kanali Mathias Kahabi Kwa kufanya Mkutano wa Hadhara ili kusikiliza na kutatua kero zao aendelee na utaratibu Ambao umewafurahisha wananchi wa Rulenge.
Naye Diwani kata ya Rulenge alisema tayari ameanza kusikiliza kero katika mikutano Mbalimbali ya wananchi ndani ya Kata ya Rulenge ,Aidha Alimpongeza sana Mkuu wa Wilaya pia Mkurugenzi Mtendaji pamoja wataalam Kwa ushirikiano mkubwa na kuwaletea Maendeleo kata ya Rulenge.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathias Kahabi akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Solomon Kimilike, katibu Tawala wilaya Bi Hatujuani Lukali na Mhe Niyonzoma Fabian wakiwa katika Mkutano wa kusikiliza na kutatua kero Rulenge.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Hadhara Oparesheni Sikiliza kero za wananchi Rulenge.
Viongozi wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara.
Wananchi.
Mkuu wa Wilaya akiwasisitiza suala usafi wa Mazingira Rulenge.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara akiwa katika picha ya pamoja na viongozi baada ya kumalizia zoezi la kusikiliza na kutatua kero Rulenge.
Diwani kata ya Rulenge Niyonzoma Fabian alkmshukuru Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa Fedha tsh Bilioni 2 .54 Kwa ajili ya miradi ya Maendeleo Mamlaka ya Mji Mdogo wa Rulenge Wilayani Ngara.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa