- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Walimu wakuu wa shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wameagizwa kuhahkikisha kila mwanafunzi katika shule hizo, amepanda mti wa matunda au wa kivuli, ambao ataukabidhi akimaliza masomo yake.
Agizo hilo limetolewa na Afisaelimu Ufundi wa Halmashauri ya Wilaya ya ngara Ndugu fidlelis Malimbu; wakati wa kikao cha kazi, kilichofanyika Machi 15, 2018, katika Ukumbi wa shule ya sekondari ya Ngara, na kuwajumuisha walimu wakuu wa shule za sekondari.
“Tumekwisha agiza kwamba kila shule ipande miti ya matunda na ya vivuli; lakini utelezaji wake umekuwa unasuasua, sasa tunawaagiza kwamba kila mwanafunzi awe na mti mmoja wa matunda au wa kivuli, atakaoukabidhi atakapomaliza shule.” Alisema ndugu Malimbu.
Amesema agizo hili ni la Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali zaMitaa (OR-TAMISEMI) si lake, hivyo kinachotakiwa ni utekelezaji na si vinginevyo.
Amewaambia wakuu hao wa shule za sekondari, kuwa ifikapo Aprili 03, 2018; kutakuwa na ukaguzi wa miti hiyo katika kila shule, kwa kuangalia idadi ya miti iliyopandwa na wanafunzi waliopo shuleni.
Amewaagiza maafisaelimu Kata Kufuatiliaa agizo hili, na kuongeza kwamba, kama shule ina wanafunzi mia nne (400), wanatarajia kukuta shule hiyo imepandwa miti kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo katika shule husika.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa