- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wakulima wa kahawa katani Kirushya katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wameishukuru serikali kwa kuwaepusha na wahujumu wa kahawa,kwa madai kwamba musimu huu wanaweza kunufaika na zao hilo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Mwivuza Ndugu BaduluhTwaha, amesema wakulima mwaka huu watanufaika na zao hili, baada ya serikalikuwapiga faini walanguzi waliokiuka agizo la kutonunua kahawa ikiwa shambani.
“Serikali ina nguvu na uwezo mkubwa bwana! kwani walewote waliokuwa wamenunua kahawa ikiwa bado shambani kwa kutanguliza fedha, hivisasa wakipewa kahawa kama fidia wanakataa wanataka warejeshewe fedha yao.”Alisema Ndugu Twaha.
Amefafanua kwamba walanguzi wa kahawa walikuwawanawadhulumu wakulima, kwani mkulima akipewa labda shilingi 300,000/= mlanguzianapata faida mara tatu ya malipo aliyomlipa mkulima.
Naye Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika (W) NduguConstantine Mudende, amekiri kwamba wakulima mwaka huu watanufaika, kwaniwatalipwa kulingana na soko la wakati huo, na kwamba kila mmoja atatamanikulima zao hili kufuatia bei nzuri.
Amesema wakulima katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngarawawe na subira, kwa madai kwamba msimu huu Ngara Famaers Cooperativewanatarajia kutumia zaidi ya bilioni mbili kununua kahawa ya wakulima wilayani humo.
Amesema wamefanya mazungumzo na Benki ya Maendeleo yaKilimo Tanzania (TADB), ili wapewe zaidi ya bilioni 02, kwa ajili ya kununuliakahawa na kwamba mazungumzo yanaendelea vizuri.
Afisa kilimo huyo wa Wilaya ya Ngara amesema msimuulitakiwa kuwa umeanza mwezi Mei 01, 2018; akaongeza kwamba wataanza kununuakahawa hiyo muda wowote kuanzia sasa.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa