- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Walimu wote katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wamekumbushwa kufanyakazi kwa bidii, weledi na uadilifu katika kutimiza jukumu la kuwafundisha na kuwalea watoto waliokabidhiwa.
Akisoma risala wakati wa siku ya kilele cha wiki ya Elimu Mei 30, 2018, kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele, Afisa Tarafa wa Tarafa ya Kanazi Ndugu Yusuph Jawabu, amewapongeza walimu kwa kazi wanazofanya.
“Nawakumbusha wazazi pamoja na wadau wa Elimu, jukumu la kuwaelimumisha watoto wilayani kwetu, ni la kila mdau; hivyo kila mwananchi katika nafasi yake anawajibika.” Alisema Ndugu Jawabu.
Aidha, alionyesha kusikitishwa na baadhi ya wananchi, wanaoshindwa kuelewa utekelezaji wa waraka wa elimu msingi bila malipo, na kwamba waraka namba 6 wa mwaka 2015, unalenga kwamba kila mtoto wa kitanzania apata elimu bila vikwazo.
Katika kutekeleza azma hiyo, serikali inatuma ruzuku ya uendeshaji wa shule za sekondari na za msingi, na kwamba utekelzaji wa waraka huo si mgumu kwani kila mdau ana majukumu yake.
Katika hili mkuu huyo wa wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele, amewaagiza watendaji katika ngazi ya Halmashauri, shule, kata na vijiji waendelee kutafsiri waraka huo kwa wananchi, ili kila mdau aweze kujua majukumu yake na kuyatekeleza.
Akisoma risala kwa niaba ya Afisaelimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Gideon Mwesiga, Afisa Taaluma (W) Ndugu Oswald Rujuba, amesema kwamba idara ya elimu tangu Januari hadi Aprili 2018, imepokea zaidi ya shilingi milioni 981 kwa ajili ya kusimamia shughuli mbalimbali shuleni.
Amempongeza Mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu John Pombe Magufuli, kwa kuanzisha mpango wa Elimu Bila Malipo, kwani mafanikio yake yanaonekana na kuongeza kwamba mwaka 2018 ofisi yake imewasajili darasa la kwanza watoto wapatao 14,071.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa