- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ngara ni wilaya iliyojaliwa vivutio vingi vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Wanyama Burigi, Maporomoko yapatikanayo Rusumo, Mapango ya Ntobeye,Mafiga matatu,Nyumba ya Chifu Balamba na vivutio vingine. Kufuatia uwepo wa vivutio hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan Bahama alitoa nafasi kwa wananchi wilayani Ngara kujifunza masuala mbalimbali ya kiutalii kwa kuwaletea huduma ya mafunzo karibu nao kwa gharama nafuu zaidi.
Wakati akitoa taarifa katika kikao cha Robo ya Kwanza cha Baraza la Madiwani 2019/2020, Mkurugenzi Mtendaji amewaomba Madiwani kuendelea kuwahamasisha wananchi wote hasa vijana kujitokeza kwani mwitikio bado mdogo ukilinganisha na ukubwa wa fursa hii ya Utalii inayolenga kunufaisha wengi.
Mkurugenzi alisema kuwa tayari alishaongea na chuo cha Utalii cha Serikali cha Arusha kwa ajili ya kutoa mafunzo,na baada ya kuwatangazia wananchi ,wengi walijitokeza na kujiandikisha lakini mwitikio umekuwa mdogo katika kulipia mafunzo hayo ambapo ni idadi ndogo tu ndio imelipia ukilinganisha na waliojiandikisha. Badda ya kulipia chuo kitakuja rasmi kwa kutoa mafunzo hayo ya muda mfupi na kuwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo.
Hii ni fursa nzuri kwa wakazi wa Ngara kwani utalii utaongeza fursa za ajira na kuimarisha uchumi wa Wananchi wa Wilaya ya Ngara.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa