- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ofisi ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, imeagizwa kuwatambua na kuwasajili upya wananchi wilayani humo, ili waweze kupata vitambulisho hivyo, kufuatia hofu kwamba wahamiaji haramu walijipenyeza katika zoezo hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Kangi Lugola ametoa agizo hilo Januari 06, 2019 baada ya kupata taarifa kwamba kuna uwezekano baadhi wahamiaji haramu kwa kusaidiawa, na wananchi wasiokuwa waadilifu walijipenyeza katika zoezi hilo, ili wapate vitambulisho hivyo.
“Zoezi la uandikishaji na utoaji vitambulisho vya taifa, litarudiwa ninazo taarifa kwamba baadhi ya wahamiaji haramu wamejpenyeza katika zoezi hilo; wengine kwa kutetewa na wenzetu wakapata vitambiulisho vya taifa.” Alisema Mh. Lugola.
Alitoa maelekezo vitambulisho vyote pamoja na taarifa zote za awali vitapitiwa upya, ili serikali ijiridhishe na kujua nani anastahili na nani hastahili kupata kitambulisho hicho; na kuwataka wale amabao hawakupata nafasi ya kujiandikisha kwa sababu mbalimbali wajiandikishe.
Wakati huo huo, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wote watakaoshiki katika uchaguzi wa serikali za mitaa na baadae mwakani (2020) uchaguzi mkuu wawe ni raia wa Tanzania na si vinginevyo.
“Wahamiaji haramu hawaruhusiwi kujihusisha katika masuala ya kisiasa, lakini ninazo taarifa kwamba kuna baadhi yao mahali fulani ni viongozi na wananchi wanabaki kulalamikia uhalali wa uaraia wao; huku baadhi yao wanaanzisha vurugu hapa nchi.” Alisema Mh. Lugola.
Muhamiaji haramu kwa mujibu wa sheria za nchi haruhusiwi kumiliki hata sentimita moja ya ardhi ndani ya nchi hii; lakini kuna wahamiaji haramu wengi wanamiliki ardhi, zaidi sana wengine wananufaika na elimu bure iliyokusudiwa kwa watanzania.
“Nimewaelekeza Kamishena wa Uhamiaji ashirikiane na Kamati za ulinzi na usalama ndani ya wiki mbili tangu Januari 05, 2019; wahakikishe wahamiaji haramu wote wanaondoka.” Alisema Mh. Lugola.
Akielekeza, katika kufanikisha zoezi la kuwabaini wahamiaji haramu kuna changamoto zake; akagiza maofisa wote wa uhamiaji kuwa makini wakati wa zoezi hilo, wasimuonee na wala wasidhulumu haki ya mtu yeyote.
Aidha, amepiga marufuku idara ya uhamiaji, kumtambua muhamiaji haramu kwa kigezo cha pua yake, urefu wake, kwa kuimba wimbo wa taifa au mwili wake/umbo lake; kwa madai kwamba maofisa hao wamefundishwa vigezo vya kiuredi vya kubaini nani raia na nani si raia.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa